Ujauzito wiki ya 35

Posted by Afya4all Admin on January 28, 2023 in Ufuatiliaji - Ujauzito


Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 35
Mtoto wako amekuwa mkubwa sana kwenye mji wake wa mimba na ni msumbufu, unaweza kupata mateke machache katika mbavu! Mtoto wako ameshaota tayari kucha za mikono na miguu. Figo zake zimekamilika na ini lake linaweza pia kusafisha baadhi ya taka.

Dalili za ujauzito wiki ya 35
Unaweza kuwa na hisia kwamba huna nafasi - mji wa mimba yako umeongezeka wigo kwa mara 1,000 zaidi ya kiasi chake cha awali na sasa upo chini ya mbavu zako. Kama ulianza ujauzito wako katika uzitowa afya unaweza kuongeza kati ya kilogramu 10 na 12.5 (22lb hadi 28lb) kwa sasa. Utakuwa hauongezeki uzito sana kuanzia sasa.

Kama nywele yako zimezidi kung`aa kuliko kawaida, zifurahie sana wakati huu kwani zitarudi kama awali muda si mrefu baada ya kujifungua. Wakati wa ujauzito, nywele yako inakuwa nzito, kwa sababu homoni huzuia kupotea kwa nywele kwa kawaida.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 35
Ikiwa umeanza likizo yako ya uzazi, chukua nafasi ya kupata wakati wa kupumzika mara kwa mara mchana. Ni nafasi ya kufanya mazoezi na mbinu za kupumua ulizojifunza.

Kwa nini usipate (pedicure)usafi wa miguu na kucha wakati umepata muda? Unaweza kugundua ni ngumu mno kufikia miguu yako sasa tumbo lako kubwa linakuzuia.

Una mawazo ni namna ganikujifungua kwako kutakavyokuwa? Ni vigumu kutabiri uzazi wa mtu yeyote utakuwaje, lakini kuna njia unaweza kujaribu kuweka udhibiti wa mazingira utakayojifungulia. Kwa mfano, kwa kuhakikisha kuwa wakati ukifika mazingira yako ya kujifungulia ni kama ulivyopanga, kuanzia hospitali utakayojifungulia, usafiri utakaoutumia, mtu wa karibu utakayekuwa nae na hata mkunga atakayekusaidia wakati wa kujifungua ni kama upendavyo .

Kama wewe ni baba mtarajiwa, jifunze kuhusu njia bora za kuwa mzazi mwenza. Soma ratiba ya uzazi na pata maarifa unayohitaji kujua juu ya siku ile kubwa ya mwenza wako kujifungua. Hii itakuondolea hofu wewe pia na kukufanya uwe na amani kwani utahitajika kuwa na msaada mkubwa kwa mama mjamzito na hasa baada ya kujifungua.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall