Ujauzito wiki ya 3

Posted by Afya4all Admin on January 27, 2023 in Ufuatiliaji - Ujauzito

Jinsi mtoto wako anavyokua katika wiki ya tatu
Mtoto wako ni kama tu mpira mdogo uliofanywa na mamia ya seli ambazo zinaongezeka mara kwa mara, na mwili wako unafanya kazi ya ziada kuzisaidia seli hizi.
Seli zinazoendelea kutengeneza kondo la mimba (placenta) zimeanza kuzalisha homoni ya HCG (Human Chorionic Gonadotropin). Homoni hii inatoa taarifa kwa ovari zako kuacha kutoa mayai na kuongeza uzalishaji wa homoni nyingine za estrogen na progesterone, ambazo zitasababisha mji wa mimba (uterus) kutokumwaga bitana yake (ukuta wa hedhi). HCG pia ndiyo homoni inayoweza kufanya vipimo vya mimba kuwa chanya. Mwishoni mwa wiki hii unaweza kuwa na uwezo wa kuchukua kipimo kimoja na kupata matokeo chanya.

Wakati huo huo, maji ya amniotiki (amniotic) yanaanza kujitengeneza katika uwazi (cavity) ambao utakuwa mfuko wa amniotiki (amniotic sac). Maji haya huwa kama mto kwa mtoto wako katika wiki na miezi ya mbele. Hivi sasa, mtoto wako mdogo anapokea oksijeni na virutubisho kutoka ukuta wa mji wa mimba yako. Hadi kufikia mwishoni mwa wiki ijayo, placenta itakuwa imekomaa vya kutosha kuchukua jukumu la kazi hii.

Dalili za ujauzito katika wiki ya tatu
Unaweza kuanza kutambua kwamba brazia yako inakukera au inakugusa gusa chuchu zako na kukupa vimaumivu au vihisia ambavyo hupendezwi navyo. Hii ni kwa sababu mimba hufanya matiti yako na chuchu kuwa na hisia zaidi. Unaweza pia kuona matiti yako yanachonyota zaidi, hii inasababishwa na mtiririko wa ziada damu.
Baadhi ya wanawake hupata hamu/tamaa ya chakula mapema katika ujauzito wao. Unaweza kutambua kwamba aina ya vyakula unavyopendelea vimebadilika, na kwamba vyakula unavyopendelea na vinywaji ghafla havitamanishi. Kuchukia chai, kahawa, pombe, vyakula vya kukaanga, na mayai ni kawaida kati ya mama wajawazito.

Homoni za mimba zinaweza pia kuwa na athari kwako, hivyo si jambo la kushangazwa kama wewe utajisikia uchovu, hali ya chini na kulia. Wakati wa mchana, unaweza kuhisi umechoka na kusinzia sinzia. Hii ni kwa sababu mwili wako unajiandaa kumsaidia mtoto wako.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya tatu
Wakati wa wiki tatu ya mimba, bado unaweza kutokuwa na uhakika kama wewe kweli ni mjamzito. Ni vigumu kujua wakati gani umepata mimba, kwani inategemeana sana na mzunguko wako wa hedhi (menstrual cycle)
Ishara ya wazi na dalili kwamba wewe ni mjamzito ni kukosa kipindi chako cha hedhi. Kama kipindi chako cha hedhi bado ni wiki moja au zaidi mbele hadi kufikia, inaweza kuwa bora kusubiri muda mrefu kidogo kabla ya kufanya kipimo cha mimba.

Wakati huo huo, kama wewe unahisi umechoka, pata mapumziko na utulivu. Kuoga kwa maji moto na matone kadhaa ya mafuta yenye harufu tulivu itasaidia kuondoa uchovu. Tumia baadhi ya losheni au manukato au mishumaa ya kunukia kujenga mazingira ya utulivu. Kama mpenzi/mwenzi wako yupo tayari kukusaidia, unaweza pia kuomba mkando (massage) laini na kutolewa mvutano wa misuli ya mwili.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall