Ujauzito wiki ya 11

Posted by Afya4all Admin on January 27, 2023 in Ufuatiliaji - Ujauzito


Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na moja
Mtoto wako sasa amekamilika kikamilifu, kutoka kichwani mpaka kucha za vidole vya miguu. Ana urefu wa kidole gumba. Vidole vyake vya mikono na miguu vimetengana na baadhi ya mifupa yake imeanza kuwa migumu.
Kwa kipindi cha miezi sita ijayo mtoto wako kazi yake kuu itakuwa kukua zaidi na kuwa na nguvu, tayari kwa ajili ya maisha nje ya mji wa mimba yako (uterus).

Dalili za ujauzito wiki ya 11
Utakua ukipata wingi wa hisia mpya kimwili sasa kwani wewe ni mjamzito, baadhi ya hisia huridhisha kidogo kuliko nyingine. Kama umeona unavuja mkojo wakati unapiga chafya au kucheka, jaribu kutokuwa na wasiwasi. Kinachosababisha kuvuja huku ni dhiki udhaifu (stress incontinence) na ni kawaida wakati wa ujauzito.
Mara baada ya mimba kutungwa, homoni husababisha tishu na misuli iliyopo kwenye sakafu yako ya nyonga (Pelvic Floor) kunyooka. Hii inaweza kusababisha udhaifu katika misuli (sphincter) ambayo hudhibiti kutolewa kwa mkojo kutoka kibofu cha mkojo.

Wakati unacheka, kukohoa, kupiga chafya au kukimbia, shinikizo ndani ya tumbo lako na kuzunguka kibofu cha mkojo huongezeka. Shinikizo hili hubana kibofu cha mkojo wako. Kwa kawaida, misuli ya sakafu yako ya nyonga husaidia kufunga kwa chini ya kibofu chako cha mkojo. Kama misuli hii ni dhaifu au haiwezi kubana kikamilifu, basi unaweza kupata tatizo kama hilo.
Habari njema ni kwamba kuna hatua unaweza kuchukua ili kuzuia uvujaji. Kufanya mara kwa mara mazoezi ya sakafu ya nyonga itaimarisha misuli inayofanya kazi kudhibiti kibofu cha mkojo. Kaza misuli ya sakafu yako ya nyonga “pelvic floor muscles” kwa sekunde 10– Hii ni ile misuli unayoibana wakati wa kuzuia mkojo au kujizuia usijikojolee pale unapokuwa umebanwa na mkojo. Rudia mara 10 na ni vyema ukafanya kwenye vipindi viwili au vitatu katika masaa 24.

Unachohitaji kufahamu kwenye ujauzito wiki ya 11
Kati ya wiki hii na wiki ya 14 ya ujauzito wako, utakuwa unafanyiwa skani ya "ultrasound”. Sababu kuu ya Scan hii ni kujua una ujauzito wa wiki ngapi, na kukadiria tarehe yako ya kujifungua kutokana na kipimo cha “ultrasound” pia kuangalia maendeleo ya mtoto wako na kuonyesha kama unatarajia mapacha, utatu au zaidi.
Unaweza kuacha kutumia virutubisho vya foliki asidi (folic acid) kutoka mwishoni mwa wiki hii, kwa sababu kiunganishi taarifa (neural tube) cha mtoto wako kitakuwa kimeshaundwa kikamilifu.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall