Huduma ya Kwanza: Mtu aliyekabwa kwenye koo la hewa - choking

Posted by Afya4all Admin on January 21, 2023 in Huduma ya Kwanza


  • Huduma ya kwanza: Mtu aliyekabwa kwenye koo la hewa - Choking


    Kukabwa kwenye koo la hewa hutokea pale kitu kinapokwenda na kubana koo la hewa kwenye koromelo na kuzuia kupita kwa hewa kuelekea na kutoka kwenye mapafu. Kwa watu wazima mara nyingi vipande vya chakula ndio husababisha. Kwa watoto wadogo mara nyingi huwa ni vitu vidogo vidogo wanavyochezea na kuvimeza kwa bahati mbaya. Kwa sababu kukabwa kwa koo huzuia oksijeni kuelekea kwenye ubongo ni vyema kupata huduma ya kwanza mara moja.

    Alama ya kimataifa ya mtu aliyekabwa koo la hewa ni mikono kuonekana imeishikilia shingo kwa nguvu. Kama mtu aliyekabwa koo la hewa hatoi ishara hii, ziangalie pia ishara zifuatazo:

    • Kushindwa kuongea
    • Kupumua kwa tabu au kwa kelele
    • Kushindwa kukohoa kwa nguvu
    • Midomo na kucha kuwa za bluu
    • Kupoteza fahamu

    Mtu aliyekabwa koo la hewa:

    Shirika la huduma ya kwanza (Red Cross) linaelekeza kutumia mfumo wa (tano kwa tano) kuweza kutoa huduma ya kwanza:
    Toa mapigo matano 5 mgongoni: kwa kutumia upande wa mkono ambao ungetumia kupiga kofi ila kwa nguvu zaidi piga mara tano mgongoni. Sehemu sahihi ya kupiga ni katikati ya mabawa mebega kwa nyuma mgongoni.
    Toa mapigo matano 5 kwenye tumbo: Toa mapigo matano ya tumboni ambayo kwa jina lingine ni kufaitilia mfumo wa Heimlich (Heimlich maneuver)
    Pishana kati ya mapigo matano mgongoni na matano tumboni: mpaka kilichokaba kimetoka na kuachia koo la hewa.

    Kuutumia mfumo wa Heimlich (Heimlich Maneuver)

    Kwa mtu mwingine:
    Simama nyuma ya mtu husika. Zungusha mikono yako kukizunguka kiuno chake. Msogeze mutu mhusika aegemee mbele zaidi kidogo.
    Tengeneza ngumi kwa mkono mmoja. Iweke ngumi hii juu kidogo ya kitovu chake.
    Ikamate ngumi hii kwa mkono mwingine. Bonyeza kwa nguvu tumboni kwa mpigo wa haraka kuelekea juu, kana kwamba unataka kumnyanyua mtu huyu juu.
    Toa mapigo haya ya tumboni mara 5, kama itahitajika. Kama kilichomkaba bado hakitoki, rudioa mzunguko wote wa tano-kwa-tano kama uluvyoelezewa awali.

    Kama upo peke yako fanya kwanza mzunguko wa mapigo ya mgongo na tumbo kabla ya kupika simu ya dharura kuomba msaada. Kama kuna mtu mwingine karibu, muelekeze mtu huyu kupiga simu kuomba msaada wakati wewe unatoa huduma ya kwanza.
    Kama mhusika ataonekana anapoteza fahamu, inashauriwa kumfanyia huduma ya kwanza ya CPR inayojumuisha kukisukuma kifua na kutoa pumzi mdomoni. (Makala nyingine inayohusu huduma hii ya kwanza itafuata baadae)

    Kwako mwenyewe:
    Kwanza kama upo mwenyewe na umekabwa koo la hewa, piga 112 au namba ya dharura ya sehemu ulipo haraka iwezekanavyo. Halafu, ijapokuwa unaweza ukashindwa kujipiga mgongoni ila bado una uwezo wa kutumia mfumo wa kupiga tumboni na kukiondoka kinachokukaba.
    Weka ngumi juu kidogo ya kitovu
    Ishike ngumi hii kwa mkono mwingine na egemea sehemu ngumu upande wa meza au egemeo la kiti itafaa.
    Iingize ngumi yako ndani ya tumbo kuelekea juu

    Kwa mwanamke mjamzito au mwenye umbile kubwa:
    Iweke mikono yako juu zaidi kuliko mfumo wa Heimlich wa kawaida, chini kidogo ya chembe cha moyo, pale mbavu za chini kabisa zinapokutana kufuani.
    Endelea kutumia mfumo wa Heimlich kwa kubonyeza kwa nguvu kuelekea kifuani, kwa mapigo ya haraka.
    Rudia mpaka chakula au kilichokuwa kimekaba kimetoka au mhusika anapoteza fahamu

    Namna ya kuifungua njia ya hewa kwa mtu aliyepoteza fahamu:

    Mlaze mtu kwa mgongo kwenye sakafu
    Fungua njia ya hewa. Kama unakiona kilichomkaba nyuma kabisa ya koo la mhusika, ingiza kidole mdomoni na ukisafishe kinachomkaba kitoke nje. Kuwa muangalifu usikisukume chakula au chochote kinachomkaba ndani zaidi, kwani inaweza kutokea kwa urahisi zaidi kwa watoto.
    Anza mapigo ya uhai (Cardiopulmonary Resescitation, CPR) kama kinachomkaba kinaendelea kumkaba na mtu haoneshi dalili ya kupata nafuu. Mapigo ya uhai ya CPR yanaweza yakasababisha kinachomkaba kikatoka. Kumbuka kuangalia mdomo mara kwa mara.

    Mtoto mdogo chini ya mwaka mmoja:
    Chuchumaa kama upo kwenye mkao wa kukaa. Mbebe mtoto kicha kikiwa kinaangalia chini kwenye mkono wako, ambao umelala juu ya paja lako.
    Mbonyeze kwa kiganja chako kichanga huyu mara tano katikati ya mgongo wake. Kwa mkao huu na mapigo haya ya mgongoni yatatosha kukiondoa kitu kinachomkaba.
    Mshike mtoto uso ukiwa unaangalia juu kwenye mkono wako, katika mkao ambao kichwa kipo chini kuliko kiwiliwili kama njia hapo juu haikusaidia. Kwa kutumia vidole viwili vilivyowekwa kwenye chembe cha moyo cha mtoto, toa mapigo matano ya kukibonyeza kifua.
    Rudia mapigo ya mgongoni na msukumo wa kifua. Kama kupumua hakutarudi. Piga simu kuomba msaada wa matibabu ya haraka.
    Anza kufanya mapigo ya uhai (CPR). Kama moja ya njia hizi zimefungua njia ya hewa lakini mtoto huyu bado hajaanza kupumua

    Mtoto mdogo juu ya mwaka mmoja:
    Toa mapigo ya tumbo pekee

    Kujiweka tayari kwa tatizo kama hili au kwa matatizo mengine ambayo huduma ya kwanza inaweza ikawa ndio msaada pekee utakaosaidia kuokoa maisha ya mtu wako wa karibu. Ni vyema ukajifunza au kujisomea kuhusu namna mbali mbali za kutoa huduma ya kwanza.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall