Drone kuanza kusambaza damu vijijini Tanzania

Posted by Afya4all Admin on January 25, 2023 in Habari na Utafiti


Zipline kuanza kufanya shughuli za kusafirisha damu kwa kutumia drone nchini Tanzania.
Kampuni ya California nchini Marekani - Zipline imetangaza rasmi nia yake ya kuanza shughuli za kusambaza damu vijijini nchini Tanzania kwa kutumia drones. Kampuni hii ilianza kutoa huduma kama hii nchini Rwanda mnamo mwaka jana na kuwa kampuni ya kwanza duniani kusafirisha damu na vifaa-tiba mbalimbali kutoka hospitali kubwa mijini na kuzipeleka vijijini kwa njia ya ndege ndogo zisizo na dereva (drone).

CEO wa Zipline alisema kuwa kupelekea mafanikio yaliyoonekana huko Rwanda, kampuni yake ikishirikiana na wizara ya afya na MSD wanategemea kujiunga na mashirika mengine matatu, Human Development Impact Fund, Bill and Melinda Gates Foundation na Saving Lives at Birth Foundation kuweza kukamilisha mradi huu unaotegemea kuanzisha vituo vinne vya kurushia drone hizi ndani ya miaka minne ijayo.

Tanzania itakuwa ni nchi ya pili sio Afrika tuu bali duniani kote kuwa na huduma hii ya kusafirisha damu, madawa na vifaa tiba muhimu kwa kutumia teknolojia ya drones.

Kampuni ya Zipline hutengeneza drone zake yenyewe na huwa na uwezo wa kusafiri hadi kilometa 150 kwa chaji moja. Drone hizi zina uwezo wa kubeba hadi kilo moja na nusu ya mzigo.

Teknolojia hii ambayo inategemea kuanza mapema mwakani itasaidia huduma za damu na dawa muhimu kufika maeneo ambayo usafiri ni wa shida na ngumu kufikika. Sehemu ambayo gari lingetumia masaa manne inaweza kufikiwa kwa drone ndani ya nusu saa. Hivyo kuokoa muda, gharama na maisha ya wagonjwa.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall