Dalili na Ishara kuu 10 kuwa una Ujauzito

Posted by Afya4all Admin on January 25, 2023 in Dalili na Ishara


1. Kuwasha na kuvuta kwa chuchu
Kadiri homoni za mimba zinavyoongeza usafirishaji wa wa damu kwenye matiti yako, unaweza kuhisi hali ya kuvuta kuzunguka chuchu zako. Hii inaweza kuwa moja ya dalili za awali za mimba, na muda mwingine kugundulika pia ndani ya wiki au zaidi ya utungaji wa mimba. Mara baada ya mwili wako kuzoea  ongezeko la homoni, hali hii itapotea.

2. Maumivu ya tumbo na kugundua kuchafuka
Sio kawaida kuchafuka ukiwa na karibia wiki 6 za mimba. Unaweza kugundua rangi ya pinki kwa mbali au madoa ya kahawia katika nguo zako za ndani(chupi) au wakati unakojoa au kuhisi maumivu ya tumbo kwa mbali. Wataalamu hawana uhakika kabisa kwanini dalili hizi zinatokea katika hatua za awali za mimba. Inafikirika kusababishwa na ukuaji wa plasenta. Kama umekumbwa na tatizo la kutokwa damu ambalo sio kawaida, muone daktari mapema ili kuwa katika hali ya usalama.

3. Kujisikia kuumwa
Kama una bahati utaepuka kichefuchefu kabisa. Hata hivyo,magonjwa ya asubuhi ni moja ya dalili za awali za kawaida za mimba, japo zinaweza kuanza mapema katika wiki ya nne. Unaweza kujisikia kuumwa na kichefuchefu. Hali hii inaweza kukupata mda wowote ndani ya siku, mchana au usiku.

4. Kukua,kuvimba kwa matiti
Mara baada ya kufika wiki ya sita ya ujauzito wako, matiti yako yanakua nyeti zaidi. Inakua sawa na jinsi unavyojisikia kabla ya hedhi. Unaweza kugundua kwamba maziwa yako yamekua na kuvimba,na mishipa kuonekana chini ya ngozi. Kukua kwa maziwa ni dalili ya kawaida katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

5. Kujisika kuchoka
Umechoka? Unaweza jikuta unashinda kitandani mda wote kadiri mwili wako unavyojitahidi kukubaliana na uwepo wa mtoto ndani yako, tangu mwanzo wa mimba. Homoni za mimba za mwili wako ndio zinakufanya kuhisi umechoka, mwenye hasira na hisia kali. Uchovu ni dalili ya kawaida ya mimba, na hutokea zaidi katika kipindi cha kwanza cha mimba na hatua za mwisho za ujauzito.

6. Uhitaji wa kukojoa kila mara
Katika wiki yako ya sita ya mimba utagundua unakojoa sana. Hii ni kwasababu ya mjumuiko wa homoni za mimba, wingi wa damu ndani ya mfumo wako na figo zako kufanya kazi ngumu zaidi. Ikiwa utahisi maumivu au kuungua wakati unakojoa, unaweza ukawa na UTI, muone daktari kama unahisi unao huu ugonjwa.

7. Chuchu nyeusi
Mabadiliko ya ngozi ni ya kawaida wakati wa ujauzito. Moja ya mabadiliko ya kwanza ambayo unaweza kuona ni mduara wa ngozi pande zote za chuchu zako (vidogo) vinakua nyeusi. Hii inaweza kutokea kutoka wiki nane. Unaweza pia kupata kwamba  vifungo vidogo vyangozi  vinavyozunguka chuchu zako vinajitokeza zaidi na kuchomoza zaidi. Vumbu yako na uke hubadilika na kua nyekundu zambarau iliyokolea, ingawa unaweza usione hili.

8. Matamanio ya chakula na kuhisi haraka kwa mabadiliko ya harufu au hisia ya harufu kubadilika.
Mabadiliko katika matamanio ya chakula yanaweza kuwa dalili ya ujauzito. Unawezekana kuacha ladha fulani wakati wa kwanza, hasa kabla hujakosa kuona hedhi yako. Unaweza kuhisi  ladha ya chuma katika kinywa chako, au kushindwa kutumia kahawa yako ya asubuhi au chakula ambacho unachokipenda, kama vile mayai. Hisia yako ya harufu inaweza pia kubadilika, mabadiliko haya yanaweza kuwa makali zaidi kwenye chakula na harufu ya mapishi.

9. Kukosa hedhi
Ikiwa hedhi yako ni ya kawaida, na hedhi yako haijaanza kwa muda, ni bora ukachukua kipimo cha mimba kabla hujagundua dalili nyingine. Kukosa hedhi yako ni moja ya ishara hakika ya ujauzito. Lakini ikiwa  hedhi yako si ya kawaida au unapoteza dira ya hedhi ijayo inakuja lini, unaweza usigundue kama hedhi yako imechelewa. Katika kesi hiyo, matiti ya kukua, hisia za kichefuchefu na kufanya safari za ziada chooni inaweza kuwa dalili za mwanzo kuwa wewe ni mjamzito.

10. Kipimo cha nyumbani cha mimba
Vipimo vingi vya mimba vya nyumbani vitakupatia majibu ya uhakika , kama ukisubiri mpaka siku ya kwanza ya kukosa hedhi yako.

author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall