Afya4All ni nini?

Afya4All.com ni tovuti inayotoa taarifa, ushauri na huduma za kiafya mtandaoni. Katika ulimwengu wa sasa hakuna sababu ya mtu kutokuwa na uwezo wa kupata taarifa za kiafya za uhakika, kiurahisi na katika wakati muafaka.

blog-post-image

Afya4All-Tovuti pamoja na Afya4All-App ni huduma mtandao zilizoanzishwa nchini Tanzania kuwakomboa wanawake na watoto wakiwa kama kundi maalumu la afya kwenye jamii. Afya4All imedhamiria kutoa taarifa, ushauri na huduma za afya kwa jamii kuhusu ujauzito, mtoto na malezi bora kwa lugha ya Kiswahili. Maamuzi ya kutumua Kiswahili ni ili kuweza kuwafikia walengwa kwa lugha nyepesi na inayoeleweka ili kuleta mapinduzi ya uhaba wa taarifa sahihi za afya na zinazopatikana kwa wakati sahihi mtandaoni.

Baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa muda mrefu za namna ambavyo huduma za kiafya zinaweza kutolewa mtandaoni, Afya4All imefungua tovuti rasmi itakayokuwa inakuletea moja kwa moja huduma hizi popote pale ulipo ukiwa umejiunga na mtandao. Pia unaweza kupata huduma hizi kwa kupakua app ya Afya4All kutoka Google Play (Android).

Ni kweli kwamba asilimia kubwa ya Watanzania kwa sasa wanatumia huduma nyingi za kimtandao, ikiwemo mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram na whatsapp. Ni wakati muafaka sasa kutumia uwezo huu wa mtandao kujifahamisha na kujiweka katika uelewa mkubwa kuhusu afya ya jamii na hasa hasa afya ya wajawazito na watoto.

Sehemu kuu tatu za Afya4All

Afya4All inategemea kuwa mtandao wako pekee na tegemezi kwenye kupata taarifa, ushauri na huduma za kiafya mtandaoni.

  • Sehemu ya kwanza inahusu utoaji wa taarifa mbalimbali za kiafya. Taarifa hizi ni za moja kwa moja na zitakuwa zinalenga makundi yote katika jamii kwa kuanzia na kundi maalumu la wajawazito na watoto.
  • Sehemu ya pili inahusu utoaji ushauri mbalimbali kuhusu makundi maalumu kwenye jamii. Ushauri huu ni wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya na utakuwa unapatikana kwa yoyote aliyejiunga na Afya4All Web au Afya4All App.
  • Sehemu ya tatu inahusu utoaji wa huduma za kiafya kwenye mtandao. Kwa kufahamu umuhimu wa makundi maalumu ya kiafya kwenye jamii. Afya4All inatoa huduma za kimtandao kuwezesha watumiaji kufuatilia hatua kwa hatua ujauzito tangu wiki ya kwanza hadi kujifungua pamoja na ukuaji wa mtoto tangu kuzaliwa mpaka mwaka mmoja. Huduma hizi zinapatikana kwa kupakua app yetu ya Afya4All na kujiunga kwani tarehe za ujauzito na kuzaliwa kwa mtoto zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

"Afya4All inategemea kukua na kuongeza huduma nyingi zaidi za kiafya mtandaoni kwa lugha ya Kiswahili kuweza kuwafikia watu wengi nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla."

Ngao yetu ya uadilifu hapa Afya4All

Hapa Afya4All tumedhamiria kutoa taarifa na huduma za afya za uhakika na zilizo sahihi kila wakati kwa lugha ya Kiswahili. Ngao zetu za uadilifu.

  • Usahihi, Kila moja ya makala zetu kati ya zote 3000+ zinapitiwa na kusahihishwa na wataalamu wetu wa afya kuhakikisha zipo sahihi na hazitaipotosha jamii.
  • Usasa, Taarifa na makala zote ndani ya Afya4All zinapitiwa mara kwa mara na zinaakisi hali ya sasa ya taaluma na huduma za kiafya.
  • Uhakika, Afya4All ni mfumo wenye uhakika unaotumia teknolojia na rasilimali watu kutoka sekta za afya na sayansi na teknolojia ya mtandao kuifikia jamii inayokitumia Kiswahili duniani kote.
Soma Zaidi