Vitu Muhimu vya Kufanya Baada ya Kujifungua

Posted by Afya4all Admin on May 5, 2022 in Ushauri na Mbinu

Omba cheti cha kuzaliwa cha mtoto sasa

Fanya kutengeneza cheti cha mwanao katika ofisi za RITA, mara utakapokipata kihifadhi vizuri na tengeneza nakala mbili alafu hifadhi. Ukiomba cheti mapema inapunguza usumbufu hapo baadae.

Omba likizo ya uzazi kama unafanya kazi

Mara baada ya kujifungua hakikisha unatoa taarifa katika uongozi wa kazini kwako ili upate haki zako kama mama mzazi ikiwemo likizo.

Tuma taarifa ya kujifungua kwako kwa ndugu,jamaa na mrafiki

Sambaza habari njema kwa watu! Kwa marafiki, ndugu na majirani.

Andika salamu za shukurani

Kama una bahati ya kubarikiwa na marafiki wengi na familia waliokujali tangu awali na kumtunuku mtoto na wewe zawadi, kumbuka kuwashukuru, ni ishara ambayo haisauliki.

Anza kujipendezesha

Anza kujipendezesha mapema ili utakaporudia maisha yako usipate shida.

Jaribu kumlaza tumboni

Anza kumlaza mtoto juu ya kifua chako na jaribu kumnyanyua kichwa chake ili akuangalie, hii itasaidia kukaza misuli ya shingo na mgongo.

Nunua nguo za uzazi

Nunua nguo kama madera, gauni kubwa zitakazokupa uhuru wakati wa kunyonyesha, sidiria za kunyonyeshea ni muhimu na chupi kubwa zisizobana.

Anza mazoezi

Si rahisi kurudia utaratibu wa mazoezi mara baada ya kujifungua, lakini kutembea kunasiadia kuinua hisia zako na mwili kurejea hali ya awali.

Kula sawa

Kula matunda mengi na mbogamboga, nafaka kama ngano, wali,shayiri, mahindi. Nafaka ambazo hazijakobolewa ni nzuri. Maziwa na bidhaa zake na protini inayotoka kwenye samaki,karanga,maharage. Epuka vyakula vya mafuta hasa kwenye mifugo.

Kunywa maji mengi

Bado kuna mengi yanayoendelea kwenye mwili wako baada ya kujifungua,kwahiyo kunywa maji mengi kutasaidia kuweka mambo sawa. Tafuta kopo zuri la maji na tembea nalo kila mahali.

Ongeza mahitaji ya mtoto

Licha ya maandaklizi ya mtoto,kuna baadhi ya vitu vinahitajika kuongezwa kama nepi au diaper na jaribu kuziweka karibu mfano bafuni,kwenye begi la mtoto, sebuleni na hata chumbani kwa mtoto.

Toka nje mara moja kwa siku

Hata kama ni kuzunguka nyuma ya nyumba, pata hewa safi itakusaidia kuondoa uchovu na mawazo.

Pata msaada kama unahitaji

Kama umechoka ongea na daktari wako. Pata msaada, ongea na  mshauri nasaa au pata matibabu ya msongo wa mawazo baada ya kujifungua,sio jambo la kuona aibu. Matatizo ya hisia baada ya kujifungua yanaletwa na mabadiliko ya homoni na haina maana wewe ni mvivu, kichaa au mama mbaya.

Mjue mwanao

Hili ni jambo la muhimu sana-jaribu kufurahia muda na mwanao mchanga. Ni jambo la kuchosha,kukasirisha, kuchanganya na kuleta changamoto, lakini ni jambo la muhimu sana. Sio kila mtu anafurahia kila mda lakini jitahidi kutafuta kitu kizuri kila siku.


author-avatar
Published by
Afya4all Admin

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur elit eiusmod tempor sapien dolore incidide undo labore dolore incididunt ut labore turpis vitae raesent varius efficitur ipsum primis cubilia laoreet augue egestas luctus donec diam efficitur ipsum primis in cubilia laoreet augue egestas

Related Posts:

March 11,

Integer congue magna at pretium purus pretium

An enim nullam tempor sapien gravida donec enim blandit ipsum porta justo integer odio velna vitae auctor integer

By Joel Peterson

March 04,

Congue magna eTreeks purus pretium magnis

Donec enim blandit and ipsum porta justo integer odio a velna vitae auctor an integer congue magna at pretium nulla

By Jennifer K.

February 24,

8 neque dolor primis a libero tempus blandit

Porta justo integer odio velna vitae an auctor integer congue magna at pretium purus ligula rutrum luctus risus ultrice

By Michael Deal

February 19,

Ligula varius magna and porta a laoreet pretium

Vitae auctor integer a congue magna undo pretium at purus pretium ligula a rutrum luctus risus and ultrice blandit

By Aaron Wall