Miadi ya Kliniki ya Mtoto
Posted by Afya4all Admin on May 5, 2022 in Ushauri na Mbinu
Baada ya kuzaliwaDaktari wa watoto atampima mtoto ndani ya masaa 24 baada ya kuzaliwa,
na atapima mwili mzima wa mtoto kuangalia kama mwili unafanya kazi
ipasavyo. Baadhi ya vipimo utakavyoona mwanao akifanyiwa kwanza:
Daktari atampima mwanao urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake. Vipimo hivi vitaandikwa kwenye chati ya ukuaji.
Uwezo wake wa kusikia
Kipimo cha damu kuchunguza magonjwa ya kurithi, seli mundu na mengineyo.
Pia katika kipindi hichi mtoto atapewa chanjo ya kifua kikuu (sindano bega la kulia) na polio (matone ya mdomoni).
Mwezi wa 1
Katika miadi hii ya kwanza ya mtoto wako, mtaalamu wa watoto atafanya
vipimo vya muhimu kama urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake,
fuatilia ukuaji wa mtoto,atauliza maswali ili kufanya tathmini ya hali
ya kisaikolojia/tabia ya mtoto ambayo utaifahamu kwa kuangalia matendo
na mwitikio wa mtoto wako katika mazingira mapya. Mwisho kabisa daktari
atafanya vipimo vya mwili kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole-masikio,
macho, mdomo, ngozi, moyo na mapafu, tumbo, mapaja na sehemu zake za
siri zitapimwa kuhakikisha zina afya.
Mwezi wa 2
Katika miadi hii ya mwezi wa pili, daktari atampima mtoto vipimo
muhimu urefu, uzito, na mzunguko wa kichwa chake, pamoja na tabia na
ukuaji wa mwili wake. Jambo la tofauti katika miadi hii ni mtoto
atachomwa sindano nyingi za chanjo.
Mtoto atapewa chanjo ya ugonjwa wa kupooza(matone
mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la
kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone
mdomoni).
Mwezi wa 3
Katika miadi hii, daktari atampima mtoto vipimo muhimu urefu,uzito,na
mzunguko wa kichwa chake, pamoja na tabia na ukuaji wa mwili wake.
Pamoja na chanjo za mara ya pili ya ugonjwa wa kupooza(matone
mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la
kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone
mdomoni).
Mwezi wa 4
Mtoto anakua mkubwa! Ana miezi minne sasa na muda wa kliniki
nyingine. Katika miadi hii ya nne tegemea vipimo vya kawaida kama kupima
mwili wake urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake, fuatilia ukuaji wa
mtoto,atauliza maswali ili kufanya tathmini ya hali ya
kisaikolojia/tabia ya mtoto ambayo utaifahamu kwa kuangalia matendo na
mwitikio wa mtoto wako katika mazingira mapya. Mwisho kabisa daktari
atafanya vipimo vya mwili kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole-masikio,
macho, mdomo, ngozi, moyo na mapafu,tumbo,mapaja na sehemu zake za siri
zitapimwa kuhakikisha zinaafya.
Mtoto anaweza kufanyiwa kipimo cha haemoglobini kuangalia kama ana
anemia na chanjo ya mwisho ya magonjwa ya kupooza(matone
mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la
kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone
mdomoni).
Mwezi wa 6
Mtoto kafika nusu mwaka tangu amezaliwa, miadi ya kliniki atafanyiwa vipimo vya kawaida
Miezi 9
Tegemea vipimo vya kawaida. Mtoto atapewa chanjo ya kwanza ya surua(sindano bega la kushoto)
Miezi 12
Mtoto ana umri wa mwaka mmoja, ikiwa mtoto hajapata shida yoyote ile,
tegemea vipimo vya kawaida kwa mtoto wako. Kama mtoto hajapata chanjo
ya surua ni wakati mzuri wa mwanao kupata.
Miezi 15
Kama kawaida mtoto atapimwa vitu muhimu, pamoja na chanjo ya pili ya surua.
Miezi 18
Miezi michache imebaki mwanao kufikisha miaka miwili. Kama mtoto wako
hana tatizo lolote la kiafya, katika miadi hii atafanyiwa vipimo vya
kawaida kama siku zote.
Miezi 24
Hongera mwanao ana miaka 2 sasa! Mtoto atapitia vipimo muhimu kama
kawaida na kipimo cha mwili kuangalia kama ogani zake zinafanya kazi
vizuri. Kama ana tatizo la kiafya ni wakati mzuri wa kumpeleka kwa
daktari maalumu wa tatizo husika.
Daktari wa watoto atampima mtoto ndani ya masaa 24 baada ya kuzaliwa, na atapima mwili mzima wa mtoto kuangalia kama mwili unafanya kazi ipasavyo. Baadhi ya vipimo utakavyoona mwanao akifanyiwa kwanza:
Daktari atampima mwanao urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake. Vipimo hivi vitaandikwa kwenye chati ya ukuaji.
Uwezo wake wa kusikia
Kipimo cha damu kuchunguza magonjwa ya kurithi, seli mundu na mengineyo.
Pia katika kipindi hichi mtoto atapewa chanjo ya kifua kikuu (sindano bega la kulia) na polio (matone ya mdomoni).
Katika miadi hii ya kwanza ya mtoto wako, mtaalamu wa watoto atafanya vipimo vya muhimu kama urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake, fuatilia ukuaji wa mtoto,atauliza maswali ili kufanya tathmini ya hali ya kisaikolojia/tabia ya mtoto ambayo utaifahamu kwa kuangalia matendo na mwitikio wa mtoto wako katika mazingira mapya. Mwisho kabisa daktari atafanya vipimo vya mwili kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole-masikio, macho, mdomo, ngozi, moyo na mapafu, tumbo, mapaja na sehemu zake za siri zitapimwa kuhakikisha zina afya.
Katika miadi hii ya mwezi wa pili, daktari atampima mtoto vipimo muhimu urefu, uzito, na mzunguko wa kichwa chake, pamoja na tabia na ukuaji wa mwili wake. Jambo la tofauti katika miadi hii ni mtoto atachomwa sindano nyingi za chanjo.
Mtoto atapewa chanjo ya ugonjwa wa kupooza(matone mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone mdomoni).
Katika miadi hii, daktari atampima mtoto vipimo muhimu urefu,uzito,na mzunguko wa kichwa chake, pamoja na tabia na ukuaji wa mwili wake. Pamoja na chanjo za mara ya pili ya ugonjwa wa kupooza(matone mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone mdomoni).
Mtoto anakua mkubwa! Ana miezi minne sasa na muda wa kliniki nyingine. Katika miadi hii ya nne tegemea vipimo vya kawaida kama kupima mwili wake urefu,uzito na mzunguko wa kichwa chake, fuatilia ukuaji wa mtoto,atauliza maswali ili kufanya tathmini ya hali ya kisaikolojia/tabia ya mtoto ambayo utaifahamu kwa kuangalia matendo na mwitikio wa mtoto wako katika mazingira mapya. Mwisho kabisa daktari atafanya vipimo vya mwili kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole-masikio, macho, mdomo, ngozi, moyo na mapafu,tumbo,mapaja na sehemu zake za siri zitapimwa kuhakikisha zinaafya.
Mtoto anaweza kufanyiwa kipimo cha haemoglobini kuangalia kama ana anemia na chanjo ya mwisho ya magonjwa ya kupooza(matone mdomoni),dondaakoo,kifaduro,pepopunda na hepatiti B(sindano paja la kushoto) chanjo ya nimonia(sindano paja la kulia) na kuhara(matone mdomoni).
Mtoto kafika nusu mwaka tangu amezaliwa, miadi ya kliniki atafanyiwa vipimo vya kawaida
Tegemea vipimo vya kawaida. Mtoto atapewa chanjo ya kwanza ya surua(sindano bega la kushoto)
Mtoto ana umri wa mwaka mmoja, ikiwa mtoto hajapata shida yoyote ile, tegemea vipimo vya kawaida kwa mtoto wako. Kama mtoto hajapata chanjo ya surua ni wakati mzuri wa mwanao kupata.
Kama kawaida mtoto atapimwa vitu muhimu, pamoja na chanjo ya pili ya surua.
Miezi michache imebaki mwanao kufikisha miaka miwili. Kama mtoto wako hana tatizo lolote la kiafya, katika miadi hii atafanyiwa vipimo vya kawaida kama siku zote.
Hongera mwanao ana miaka 2 sasa! Mtoto atapitia vipimo muhimu kama kawaida na kipimo cha mwili kuangalia kama ogani zake zinafanya kazi vizuri. Kama ana tatizo la kiafya ni wakati mzuri wa kumpeleka kwa daktari maalumu wa tatizo husika.