Mbinu za Kuifanya Nyumba Yako Salama kwa Mtoto
Posted by Afya4all Admin on May 5, 2022 in Usalama
Bafuni:Kamwe usimuache mwanao ndani bafuni au kwenye maji mwenyewe. Kumbuka
inachukua dakika chache mtoto kuzama na kufariki ndani ya maji, kuliko
vile unafikiria. Hakikisha vitasa vya chooni na bafuni vinafungwa vizuri
ili kufanya ugumu mwanao kufungua. Kila mara hakikisha sakafu ya chooni
na bafuni ni kavu.
Samani nzito:
Kama meza, kiti, kabati. Hakikisha samani hizi zimewekwa katika hali ya usalama ili kuepuka kuhatarisha usalama wa mtoto.
Kabati:
Kawaida kabati hatuweki vitu salama. Dawa za kusafishia choo na bauni
au vyombo jikoni, sabuni za unga na maji na bidhaa nyingine amabazo ni
hatari kwa afya ya mtoto. Hakikisha unaondoa bidhaa na vyombo hatari
kwenye makabati amabyo mwanao anaweza kufikia au kumbuka kufunga
makabati hayo na funguo.
Ngazi:
Ikiwa nyumba yako ina ngazi, hakikisha kuweka geti dogo litakalomzuia mtoto kuzifikia ngazi na kudondoka.
Jikoni:
Katika sehemu ambazo ni hatari sana kwa mtoto ni jikoni. Jikoni kuna
vitu vyenye ncha kali kama visu, pia jikoni kuna hatari ya moto sanasana
wakati wa kupika. Pia kama kuna friji (jokofu) kuna hatari ya mtoto
kuchezea na kuingia kwenye friji. Ni vyema kuhakikisha mlango wa jikoni
unakuwa umefungwa wakati wote kuepuka hatari hizi.
Kamwe usimuache mwanao ndani bafuni au kwenye maji mwenyewe. Kumbuka inachukua dakika chache mtoto kuzama na kufariki ndani ya maji, kuliko vile unafikiria. Hakikisha vitasa vya chooni na bafuni vinafungwa vizuri ili kufanya ugumu mwanao kufungua. Kila mara hakikisha sakafu ya chooni na bafuni ni kavu.
Kama meza, kiti, kabati. Hakikisha samani hizi zimewekwa katika hali ya usalama ili kuepuka kuhatarisha usalama wa mtoto.
Kawaida kabati hatuweki vitu salama. Dawa za kusafishia choo na bauni au vyombo jikoni, sabuni za unga na maji na bidhaa nyingine amabazo ni hatari kwa afya ya mtoto. Hakikisha unaondoa bidhaa na vyombo hatari kwenye makabati amabyo mwanao anaweza kufikia au kumbuka kufunga makabati hayo na funguo.
Ikiwa nyumba yako ina ngazi, hakikisha kuweka geti dogo litakalomzuia mtoto kuzifikia ngazi na kudondoka.
Katika sehemu ambazo ni hatari sana kwa mtoto ni jikoni. Jikoni kuna vitu vyenye ncha kali kama visu, pia jikoni kuna hatari ya moto sanasana wakati wa kupika. Pia kama kuna friji (jokofu) kuna hatari ya mtoto kuchezea na kuingia kwenye friji. Ni vyema kuhakikisha mlango wa jikoni unakuwa umefungwa wakati wote kuepuka hatari hizi.